Posts

Showing posts from 2016

Serikali imepiga stop kumzungumzia Faru John soma zaidi hapa

Image
     Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani amesema kuwa hakuna mwenye Mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusu faru John kwa sasa zaidi ya Waziri Mkuu kwa kuwa jambo hilo liko chini ya ofisi yake. kwaajili ya uchunguzi. Ameyasema hayo Wilayani Ngorongoro katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili wilayani humo kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyo yatoa hivi karibuni akiwa Arusha. “Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakae weza kutoa ripoti hii nje kwaajili ya matumizi ya kila mmoja wetu kwa maana ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine ya serikali yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili.”amesema Makani. Hata hivyo, Makani amesema kuwa wanasubiri maagizo au maelekezo na mwelekeo wa sasa juu ya jambo hilo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Msajili Mkuu wa Mahakama awataka mahakimu wazingatie haki ya dhamana

Image
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati amewataka mahakimu nchini kuzingatia sheria katika utendaji wao wa kazi hasa katika utoaji wa dhamana.  Kauli ya Msajili imekuja wakati kukiwa na malalamiko dhidi ya baadhi ya mahakimu kuwanyima dhamana washtakiwa ilhali mashtaka yao yanaruhusu.  Aidha, kauli ya msajili huyo mkuu imekuja wakati mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakipambana ili mteja wao apate dhamana baada ya kukwaa kisiki katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.  Mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria dhamana zake zimezuiwa ni ya mauaji ya kukusudia, uhaini, utakatishaji wa fedha, wizi wa kutumia silaha, usafirishaji binadamu na dawa za kulevya.  Hata hivyo, Mahakama inaweza kuzuia dhamana endapo kutakuwa na pingamizi la kisheria, na mara nyingi mapingamizi hayo yamekuwa yakiambatana na hati kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).  Msajili huyo alitoa maagizo hayo jana mjini Moshi alipokuwa akizungumza na mahakim

Vichwa vya magazeti ya Leo Desemba 31

Image

GRAPHICS DESIGNS

Image
If you want to get a different cover follow this blogs design  by IT_ZAHORO