Watanzania hutafuta nini mtandaoni?


Kampuni ya Google imetoa ripoti ya mambo ambayo Watanzania walitafuta sana mtandaoni mwaka 2016.
Maelezo waliyotafuta yameangazia masuala ya afya, biashara na fedha na pia burudani.
Pia, yapo masuala ya kijamii.
Walichotafuta sana mtandaoni ni matokeo ya darasa la saba 2016, zikifuatwa na Beka Boy, mtandao wa burudani.
Walitafuta pia Mkekabet, ambao ni mtandao wa kuweka dau kuhusu matokeo ya mechi za kandanda na mashindano mengine ya kimichezo.
Walitafuta pia habari kuhusu matokeo ya kidato cha nne 2016, pamoja na Raymond, ambapo walitaka habari na maelezo kumhusu mwanamuziki Hekima Raymond mzaliwa wa Moshi, Tanzania.

Walitaka kujua kufanya nini?

Watanzania walitaka sana kujua jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni, ikifuatwa na jinsi ya kuwapata wawekezaji na wafadhili.
Walitaka pia kujua sana jinsi ya kukuza nyusi na pia jinsi ya kujua mwanamke atajifungua tarehe gani.
Huenda kukoroma likawa tatizo linalowasumbua wengi kwani, kwenye nambari tano, Watanzania walitaka kujua jinsi ya kuacha kukoroma.

Kujua maana

Katika maneno ambayo Watanzania walitafuta sana maana, nambari tatu kuna neno la kushangaza 'Bae'.
Ni ufupisho wa neno 'Babe', mtoto au mpenzi kwa Kiingereza. Pia ni akronimi ya before anyone else, kabla ya wengine wote.
Kuna wimbo wa Sauti Sol na Alikiba kwa jina Unconditionally Bae, ambao huenda uliwafanya wengi kutaka kujua maana ya 'Bae'. Chanzo bbc swahili.com

Comments