Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha....

Utafiti huo uliofanywa na chuo cha masuala ya uchumi cha London ulitokana na majibu kutoka kwa watu 200,000
Afya nzuri ya akili na kuwa na mpenzi huwafanya watu kuwa kwenye furaha kuliko hata kuongezwa mshara mara dufu, kwa mujibu utafiti mpya.
Utafiti huo uliofanywa na chuo cha masuala ya uchumi cha London ulitokana na majibu kutoka kwa watu 200,000, kuhusu ni kwa njia ipi masuala tofauti huchangia maisha yao.
Kwa vipimo kutoka namba moja hadi kumi, kuongezwa mara dufu mshajhara wamtu hukumonga furaha alama ilisyo chini ya 0.2.
Hata hivyo kuwa na mpenzi kulichangia furaha kuongezeka kwa alama 0.6 na kumpoteza mpenzi kwa kutengana au kifo nako kulisababisha furaha kupungua kwa alama kama hiyo.
Madhara zaidi yalisababishwa na msongo wa mawazo ambayo ilisababisha viwango vya furaha kudidimia kwa alama 0.7. Ukosefu wa ajira pia kulichangia kushuka kwa alama sawa na hizo.
Mmoja ya waandishi wa ripoti hiyo Prof Richard Layard, anasema kuwa matokeo hayo yana maana kuwa, nchi zinastahili kuelekeza majukumu mapya kuboresha furaha kwa watu wake badala ya kuangazia njia za kukuza utajiri.
Aliongeza kuwa vitu ambavyo huchangia katika furaha zetu na kwa hatma yetu ni mahusiano na hali zetu kiafya. Chanzo bbc swahili.com

Comments