Mbunge wa Singida Mashariki Mh.Tundu Lissu apigwa risasi na watu wasiojulikana

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ameripotiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Mjini Dodoma.
Mbunge huyo amekimbizwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma General.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea akiwa naenda kupata chakula cha mchana nyumbani kwake.
Chama hicho kimeshutumu vikali tukio hilo.
Hivi karibuni, mbunge huyo kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA, amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanya uchochezi.
Akithibitisha tukio hilo,kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema " yupo hospitali, bado anajaribu kupambana kuokoa maisha yake"

Comments

Popular posts from this blog

Rais Dr John Pombe Magufuli atembelea kijiwe Cha Zamani huko Chato na kupiga stori na Vijana wa Kijiwe hicho...