Vijana Wafariki Baada Kugongwa na Train Walipokuwa wakijaribu Kupiga Selfie Mbele ya Train..


Vijana wawili wamefariki walipokuwa wanajipiga picha katika barabara ya reli katika mji mkuu wa India Delhi.
Kundi la vijana lilikwenda katika kituo cha reli kupiga selfie mbele ya treni zilizokuwa zinawadia.
Lakini wawili walichelewa kuondoka katika reli hiyo na treni ikawakanyaga, polisi imesema.
Utafiti mwaka uliopita umeonyesha kuwa kumeshuhudiwa vifo vingi vinavyohusisha watu kupiga Selfi India kuliko nchi nyingine yoyote.
Wasomi kutoka chuo kikuu cha Carnegie Mellon na taasisi ya mawasiliano ya Indraprastha mjini Delhi wanasema kuwa kati ya vifo 127 vinavyotokana na watu kupoiga Selfie kati ya mwaka 2014 - 2015, visa 76 vimeripotiwa India.
Tukio la hivi karibuni limejulikana baada ya vyombo vya habari katika eneo hilo kutoa taarifa Jumanne.

Comments