Iran kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo vipya vya Marekani

Iran imeshutumu vikwazo vipya ilivyowekewa na Marekani na kuahidi kuchukua hatua za kulipiza kisasi.
Serikali ya Washington inasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia jaribio la kombora lililofanywa Jumapili, ambalo Marekani imesema ni hatua ya Iran ya kuwasaidia magaidi katika shughuli zao mbovu duniani.
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Iran ilisema kuwa vikwazo hivyo vinakiuka mkataba ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambap ulikubali kupunguza kasi ya kuimarisha shughuli zake za kinulikia.

   Waziri Wa Mambo Ya Kigeni wa Iran Javad Zarif

Iran ilisema kuwa itawawekea watu fulani wanaoshukiwa kushirikiana na makundi ya kigaidi vikwazo na pia dhidi ya kampuni zingine za Marekani.

Marekani ilisema kuwa vikwazo vyake vitalenga kampuni 12 na watu 13 nchini Iran na kwingineko.

Comments