Waziri Nape Amvaa Makonda Sakata la Dawa za Kulevya........


Nape aasa "Tusiwahukumu watu kwa Tuhuma, kubomoa brand ya mtu/taasisi ni sekunde"

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, N. Nnauye amesema wizara yake inaunga mkono mapambano dhidi ya unga kwani kwa namna moja ama nyingine yanadhoofisha nguvu kazi ya vijana. Kama Wizara Tunaunga mkono juhudi za kupambana na jambo hili.

Lakini

Hizi ni baadhi ya nukuu za Nape:
 'Lazima itumike busara, tusiwahukumu watu kwa tuhuma,kutengeneza brand ni kazi kubwa sana wakati kuibomoa ni jambo la sekunde tu'

'Kama Wizara tunaunga mkono juhudi za kupambana na dawa za kulevya, tatizo ni namna ya kushughulika na wahusika ikiwemo busara'
 'Tunaunga jitihada za mapambano lakini ni vizuri lifanywe katika namna ya kulinda haki ya mtuhumiwa ili heshima yake isipotee'
'Nakiri kwamba tatizo la dawa za kulevya ni kubwa, watumiaji ni wengi lakini wanaoonekana zaidi ni wale wenye majina makubwa'

'Muhimu sana kulinda haki na suala la utaratibu uliotumika kwa watuhumiwa wa madawa niiachie jamii iendelee kujadilimwafa

Comments