Popular posts from this blog
Vijana Wafariki Baada Kugongwa na Train Walipokuwa wakijaribu Kupiga Selfie Mbele ya Train..
Vijana wawili wamefariki walipokuwa wanajipiga picha katika barabara ya reli katika mji mkuu wa India Delhi. Kundi la vijana lilikwenda katika kituo cha reli kupiga selfie mbele ya treni zilizokuwa zinawadia. Lakini wawili walichelewa kuondoka katika reli hiyo na treni ikawakanyaga, polisi imesema. Utafiti mwaka uliopita umeonyesha kuwa kumeshuhudiwa vifo vingi vinavyohusisha watu kupiga Selfi India kuliko nchi nyingine yoyote. Wasomi kutoka chuo kikuu cha Carnegie Mellon na taasisi ya mawasiliano ya Indraprastha mjini Delhi wanasema kuwa kati ya vifo 127 vinavyotokana na watu kupoiga Selfie kati ya mwaka 2014 - 2015, visa 76 vimeripotiwa India. Tukio la hivi karibuni limejulikana baada ya vyombo vya habari katika eneo hilo kutoa taarifa Jumanne.
Rais wa Mexico amrejesha waziri aliyemtimua
Mshirikishe mwenzako Image caption Rais Enrique Pena Nieto Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, amemteua waziri wa zamani wa fedha Luis Videgaray kuwa waziri wa mambo ya nje. Awali Luis alifutwa kazi kufuatia ziara nchini Marekani muda mfupi baada ya kuteuliwa kwa Donald Trump. Akizungumzia uteuzi huo huo wa waziri aliyekuwa amemfukuza kazi,Rais Nieto anasema amechukua hatua ili kupitia waziri huo mpya wa mambo ya nje kuweza kuimarisha mahusiano na ujio wa Rais wa Marekani Donald Trump


























Comments
Post a Comment