Wanajeshi 14 wa JWTZ Wauwawa Kongo DRC
Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba walinda amani 14 wa muungano huo waliuawa na wengine 53 kujeruhiwa baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kati ya waliouawa, angalau wanajeshi 12 walitoka Tanzania. Katibu mkuu huyo ameshutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita. Ameitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa. Wanajeshi zaidi wametumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi. Bw Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni "Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC. "Taarifa za mwanzo mwanzo eneo la shambulio eneo la Kivu Kaskazini zinaone...


































Comments
Post a Comment